My Authors
Read all threads
SAMUEL LEROY JACKSON muigizaji alie cheza filamu nyingi zaidi kuliko muigizaji yoyote hollywood, anae ongoza kwa mauzo zaidi na kuingiza pesa nyingi zaidi na ndo muigizaji mwenye asili nyeusi mwenye tuzo nyingi zaidi. Samuel Leroy Jackson Alizaliwa mnamo December 21 1948 katika
katika jiji la Washington D C akiwa kijana wapekee wa mwanamama Elizabeth Harriet and Roy Henry Jackson alikulia zaidi katika mitaa ya Chattanooga , Tennessee. Baba alikuwa akiishi mbali na familia yao katika mji wa Kansas City , Missouri na baadae alifariki kwa matumizi ya pombe
kupita kiasi, Samuel alibahatika kukutana na baba yake Mara mbili tu katika kipindi chote Cha Uhai wake na hivyo kulelewa zaidi na mama yake aliekuwa akifanya kazi kiwandani na baadae akawa anafanya kazi za ununuzi wa vitu kwa ajili ya kituo Cha Watu Wenye matatizo ya akili.
Kutoka na vipimo vya DNA Samuel Jackson alijigundua asili yake ni kutoka bara la Africa nchini Gabon, na kutokana na majibu ya uchunguzi huo alipewa uraia wa nchi hiyo Kama mzawa. Samuel Jackson anatatizo la kigugumizi toka akiwa mdogo lakini alijifunza kuweza kuongea Kama mtu
asie na kigugumizi na Mara nyingi hutumia neno "motherfucker" kuondoa kigugumizi pale kinapo mshika.

Mwanzoni alikuwa na malengo ya kusoma kozi za Marine Biology, Ila baadae alibadirisha na kuchukua masomo ya architecture kabla ya kubadili tena na kuamua rasmi kusoma masomo ya
sanaa na uigizaji, na alianza kupenda uigizaji baada ya kujiunga na Kikundi cha uigizaji chuoni ili kujipatia Alama za ziada darasani na uko akatokea kupenda shughuli za uigizaji zaidi.

Mwaka 1969 Samuel Jackson pamoja na wanafunzi wengine waliwateka wawekezaji wa chuo cha
Morehouse College, wakishinikiza mabadiliko katika mitahara ya shule pamoja na uongozi, chuo baadae kirikubaliana na matakwa hayo na kubadilisha sera zake. Lakini Samuel alishitakiwa kwa makosa ya kuwashikiria Watu kinyume Cha Sheria alichukuliwa hatua na akasimamishwa masomo
yake kwa kipindi cha miaka miwili. Lakini baadae alirejea na kumalizia masomo yake ambapo ali hitimu Mwaka 1972

Mwaka 1976 Samuel Jackson akiwa ameisha fanya kazi kadhaa ndogo ndogo za maigizo ambapo aliamua kuhama kutoka Atlanta na kwenda new York City akiwa bado anafanya kazi
za maigizo madogo Madogo hasa ya majukwaani, Jackson akijiingiza Kwenye matumizi ya pombe na madawa ya kulevya aina ya cocaine kupitiliza (addictions). Akiwa bado anapewa na kuonekana Kwenye nafasi ndogo ndogo Kama Kwenye movie 'Coming to America' Samuel Jackson alikuwa mentored
na mkali Morgan Freeman.

1990 akiwa Mara kadhaa ameisha tumia madawa kupitiliza kiasi (overdose) Samuel Jackson anaamua kuachana na matumizi ya madawa na familia yake Ikaamua kumpeleka Kwenye kituo cha kujisafisha na kuachana kabsa na matumizi ya madawa ya kulevya
(rehabilitation clinic). Baada ya kufanikiwa kujisafisha na kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya, Samuel alirejea mtaani na kuendelea na shughuli zake za uigizaji, kwanza alionekana Kwenye movie ya 'Jungle Fever' akiigiza Kama mtumia madawa kupitiliza (drug addict). Filamu
Filamu hiyo ilipendwa Sana na kusifiwa ambapo tamasha la 'Cannes Film Festival' walianda tuzo kwa ajili yake pamoja na kwamba alicheza Kama muhusika msaidizi (supporting actor).

Mwaka 1993 muongozaji nguli Quentin Tarantino alimuomba Samuel Jackson kuigiza Kwenye movie
'Pulp Fiction' ambapo uhusika wake Kwenye movie hiyo ulikuwa umeandaliwa maalumu kwa ajili yake. Pamoja na kwamba Hii ilikuwa ni movie yake ya 13 tayari. Lakini uhusika wake katika movie hii kulimfanya Sasa rasmi Samuel Jackson kutambulika duniani nakupata sifa mbalimbali kutoka
kwa wachambuzi wa movies, kutokana filamu hiyo aliweza kuwa nominated katika tuzo za Golden Globe kama Best Supporting Actor, pia alifanikiwa kushinda tuzo ya BAFTA Award Kama Best Supporting Role.

Baada ya Pulp Fiction Samuel Jackson alipewa script kadhaa kuzipitia na pia
alicheza filamu Kama Kiss of Death, The Great White Hype na Losing Isaiah filamu ambazo hazikufanya vizuri sana na alianza kupata sifa hasi kutoka kwa wachambuzi ambao wamlimsifia sana mwanzo. Lakini Hii ilifika kikomo pale alipo cheza tena kwenye movie Die Hard With a Vegeance
akiwa pamoja na Bruce Willis pamoja na movie ya Time to Kill Ambayo alicheza Kama baba alie shitakiwa kwa kosa la muaji ya wanaume wawili walio mbaka binti yake, kwa movie ya "A Time to Kill" Samuel Jackson alipata tuzo ya NAACP Image Kama Best Supporting Actor na nomination ya
tuzo za Golden Globe, na baada ya apo Samuel akawa star mkubwa wa box office na kufanya kazi nyingine kadhaa zilizofanya vizuri pia.

June 13, 2000 Samuel Jackson alitunukiwa nyota ya heshima ya Hollywood Walk of Fame. January 30, 2006 alipewa nishani ya heshima katika sherehe
za hand and footprint za Grauman's Chinese Theatre na kumfanya kuwa mtu wa Saba mwenye asili ya rangi nyeusi kupewa nishani hiyo na wa 191 katika waigizaji kutambulika kwa namna hiyo.

Katika kazi zake za uigizaji Samuel Jackson ameisha igiza na wanamuziki wa hip hop kadhaa Kama
Tupac Shakur(Juice), Queen Latifah (Juice/sphere/Jungle Fever), Method Man (One Eight Seven), LL Cool J (Deep Blue Sea/S.W.A.T), Busta Rhymes (Shaft), Eve (xXx), Ice Cube (xXx: State of the Union), Xzibit (xXx:State of the Union), David Banner (Black Snake Moan) na 50 Cent
(Home of the Brave) kwa kuongezea Samuel Jackson amecheza movie Tano na Bruce Willis.

February 2009 Samuel alisign mkataba na marvel wa kuchezs movie tisa na mpaka sasa ameisha onekana Kwenye movie 11 za Marvel Cinematic akionekana kwa Mara ya kwanza kwenye Iron Man 1 na kama
moja ya wahusika kwenye Iron Man 2.

Neilson E.C.I ambayo hufuatilia taarifa na waigizaji katika Box Office wanasema Samuel Jackson ndo muigizaji alionekana Kwenye movie nyingi zaidi ya muigizaji mwingine yoyote Hollywood akiwa amecheza na kuonekana Kwenye filamu zaidi ya 150,
ambapo mauzo yake ya ndani tu yanakadiliwa kufika dola$1.7 billion. Kufikia 2011 filamu zote ambazo Samuel Jackson alicheza Kama muhusika mkuu ama muhusika msindikizaji kwa pamoja zilikuwa zimeingiza jumla ya dola $2.81 mpaka $4.91 billion, na Hii kumfanya kuwa muigizaji wa saba
mwenye mauzo zaidi Kama muhusika mkuu na muigizaji wa pili mwenye mauzo zaidi kama muhusika msindikizaji nyuma ya muigiza sauti Frank Welker. Kulingana na kitabu cha The Guinness World Records ambacho hutumia kikokotoo Cha tofauti Kidogo kutambua kiwango cha mauzo cha waigizaji
katika Box office wanasema, Samuel Jackson ndo muigizaji mwenye mauzo zaidi duniani akiwa kaingiza kitita Cha dola $7.42 billion katika filamu zake 68 tu.

Mwaka 1980 Samuel Jackson alifunga ndoa na mwanamama LaTanya Richardson ambaye walikutana akiwa bado anasoma chuo cha
Morehouse College, na walijaaliwa kupata mtoto wa kike Zoe aliezaliwa Mwaka 1982.

Mpaka sasa Samuel Jackson ameisha kuwa nominated mara 86 kwenye tuzo mbalimbali na kaisha jinyakulia jumla ya tuzo 38 akitajwa kuwa na utajiri wa dola $250 million.
Kutokana na kuwa muigizaji pendwa zaidi akiwa kapewa hadi A.K.A ya "Cool Man" leo nikaona ni vyema tukipata wasaa adhimu wa kumjua na kumfahamu kwa undani kidogo mkali huyu na hasa ukizingatia rekodi yake katika tasnia nzima ya uigizaji.
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Cipherdot Series And Movies

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!