My Authors
Read all threads
KIONJO CHA JUMAPILI

MJUE IP MAN
Kabla ya kesho hatujakuletea Kisa cha Ugomvi kati ya Dwayne Johnson (the Rock) Na Vin Diesel katika filamu za fast and furious leo tungependa tukupe historia fupi ya IP Man anayeigizwa katka filamu za Ip Man 1- 4 na mkali Donnie Yen. Image
Watu wengi wamekuwa wakiziona na kuzitizama filamu za IP MAN kama tu filamu zingine za mapigano ya kufurahisha. Lakini filamu hizi zinaongelea historia ya master wa Martial art aliyewahi kuishi kunako miaka ya 1893 hadi 1972. Master huyu alikuwa anaitwa YIP MAN aliyezaliwa tarehe Image
1 Octoba 1893 na kufariki tarehe 2 Decemba 1972, miezi 7 kabla ya kifo cha Bruce Lee, Alikuwa master wa staili ya mapigano ya aina ya WING CHUN ambaye alifundisha wanafunzi wengi akiwemo mtu maarufu tunayemfahamu wote marehemu Bruce Lee. Ip Man alizaliwa na Ip Oi-dor na Ng Shui Image
kama mtoto wao watatu katka watoto wanne. Alikuwa na kulelewa na familia ya kitajiri katika mji wa Foshan, Guangdong na alipata elimu ya kimila akiwa na kaka yake na dada yake pia.
Katika mpango mzima wa Ip kupata maujuzi katika kupigana ulianza akiwa na umri wa miaka 9 au 13 Image
hakuna taarifa iliyokamili kuhusu hili. Lkn akiwa na umri usiopungua miaka 9 na usiozidi mika 13 maujuzi haya aliyapata kutoka kwa masta aliyeitwa CHAN WAH- SHUN, wakati Ip anajiunga na Chan alikuwa mwanafunzi wa 16 ktk wanafunzi aliowahi kuwafundisha na akawa mwanafunzi
wa mwisho kwa mzee huyo, kwani kwa wakati huo Masta Chan alikuwa na umri wa miaka 57, kitu kilichopelekea Ip kutomfaidi sana mzee huyo kwani baada ya miaka 3 baadae Masta Chan mwaka 1909 alipata kiharusi (Stroke) na kurudi kijijini kwao, Baada ya tukio hili
lililompa pigo Ip Man akalazimika kuendelea na mafunzo chini ya mwanafunzi aliyekuwa bora wa Masta Chan aliyeitwa Ng Chung-sok

Ip kufikia umri wa miaka 16 kwa msaada wa ndugu yake Leung Fut-ting alihamia Hong Kong na kusoma katika shule ya mtakatifu Stephen katika masomo yake ya
shule iliyokuwa inapokea watoto wa matajiri kutoka nje ya nchi na familia zenye utajiri zilizokuwa zinaishi Hong Kong.

Ip akiwa anaendelea na mazoezi makali sana ya mapigano katika staili ya Wing Chun na kwa kipindi chote hakuwahi kupigwa na mtu
yoyote aliyejaribu kupigana naye iwe kimchezo au kiugomvi, kutokana na sifa hii miezi 6 baadae baada ya kahamia kwenye shule yake mpya Hong Kong mwanafunzi mwenzake darasani aliyitwa LAI alimwambia Ip Man kuwa kwa kipindi hicho nyumbani kwao wanaishi na rafiki wa baba yao ambaye
ni mtaalamu sana wa Kung fu na alitoa Ofa ya mapigano ya kirafiki kati yake na Ip Man kama atapendezewa, ikumbukwe hadi kufikia siku hii anapewa ofa hii Ip Man hakuwahi kupigwa wala kushindwa pambano lolote, ofa hii ilimchanganya sana Ip Man na kufanya kuisubiri siku ya pambano
lao kwa hamu sana. Siku ya jumapili jioni Ip man akiwa na furaha kubwa ya kupata angalau mtu wa kupambana naye alifika nyumbani kwa akina Lai. Na baada ya kubadilisha mawazo kwa muda mfupi muda wa pambano lao ukawadia,
Pambano lilipoanza round ya kwanza Ip Man alipigwa kwa speed ambayo hakuielewa kabisa kitendo kilichomfanya aombe round ya pili na huku akiwa haamni kuwa anaweza kupigwa kiboya hivyo, Round ya pili ilivyoanza Ip man alijikuta kapigwa tena kwa mara ya pili tena hapa alipigwa
Huyu mtu aliyempiga Ip Man alikuwa ni mtoto wa masta aliyemfundisha masta wa ip Man (Chan wah-shun) aliyeitwa Leung Bik na baba ambaye alikuwa masta wa wote hawa alijulikana kama Masta Leung Jan.
Ip Man baada ya kupigwa alikata tamaa na aliondoka bila kuaga, aliumizwa sana na kushindwa kwake hata alikuwa hawezi kuwaambia watu kuwa alikuwa anacheza martial Art,
Week moja baada ya Ip Man kupigwa Lai alimwambia kuwa mtu uliyepigana naye (Leung Bik) anakuulizia na angependa
akuone Lakini Ip man kwa aibu alikataa kwani alijisikia vibaya sana kwenda kwa mchizi ilikuwa kama kwenda kwa mpenzi aliyekuacha akiwa na mwanaume wake mwingine, Lkn Lai alimwambia kuwa mapigano yako na mbinu zako zilimfurahisha sana Leung Bik na pia
akamfungulia siri kuwa aliyepigana naye ni mtoto wa masta aliyemfundisha masta wake hivyo anaomba kama mngeweza kuonana,
Baada ya kusikia haya yote Ip Man alipata nguvu na aibu kupungua akaenda kumuona mchizi na wakaaza tizi pamoja hadi mnamo 2011 kifo kilipomfika Leung Bik,
baada ya hapo Ip akarudi kwao Foshan mwaka 1917 akiwa na umri wa miaka 24 na akawa polisi hapo foshan ambapo aliwafundisha maaskali wa chini yake, marafiki, na ndugu lkn hakufungua chuo
Baadae Ip Man alioa na kupata watoto wanne wawili wa kike na wawili wa kiume
Jambo la kusikitisha kwa Ip Man, mke wake na binti yao walipotezana milele baada ya mke kwenda Hong Kong kwa muda, ilikuwaje hadi hili kuwafika mwaka 1951 mpaka kati ya China na Hong Kong ulifungwa aliebaki foshan akabaki huko na waliobaki hong kong wakabaki hong kong hakuna
kuonana

Hizi filamu zote za Ip Man kuanzia Ip Man 1 hadi Ip Man 4 zote kwa pamoja zinajaribu kuokota vipande vidogovidogo sana vya historia ya maisha yake. Mapigano na Tabia unayoina kwa Donnie Yen ambaye ndiye kacheza na kuuvaa uhusika kama YIP Man au
Ip Man ni tabia halisia za Ip Man Mwenyewe, ukimya wake ,upole wake na utulivu uliokithiri kwenye mapigano yake, na mengineyo uyaonayo afanyanyo Donnie Yen yanaangazia tabia halisia za Ip Man
Kionjo hiki kimewajia kutoka CIPHERDOT SERIES AND MOVIES Dodoma Image
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Cipherdot Series And Movies

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!