My Authors
Read all threads
My love or my friend. Thread

Ilikuwa kitambo nilipoanza masomo ya chuo kikuu,
nilikuwa mgumu, lakini ugumu wangu ulisababishwa na kusoma shule za wavulana ulionipelekea kupenda kujitenga na wasichana.
Ilikuwa siku ya kwanza kabisa chuoni orientation, twende sawa 😊
Nilikaa nyuma kabisa ya ukumbi uliokuwa unafanyikia semina, nilifanikiwa kuona watu wote waliopo ukumbini, wasichana wazuri na wavulana watanashati. Sura zao hazikuficha furaha walionayo kufika level hii kubwa ya elimu kwao.
Sehemu ambayo nilikaa kiti cha nyuma kabisa ya ukumbi pembeni palikuwa na mlango wa kutokea. Hivyo semina ilipoisha asilimia kubwa ya wanafunzi walipitia mlango huu isipokwa staff member ambao walitokea mlango mwingine.
Baada ya kupita wanafunzi wengi sana mwishoni walibaki
Wanafunzi wawili, wakike na wa kiume. Walionekana kama wanafahamiana kwani walikuwa wakipiga story tofauti na wanafunzi wengine waliopita. Huyu msichana alikuwa nzuri alivalia mavazi mujarabu yenye asili ya kitanga. Alionekana anasura ambayo ilionesha alikuwa na asili ya kiarabu.
Bahati mbaya walipokaribia kutoka yule mwanamke aliangusha simu. Kila kitu si kikamwagika pale chini, kava na betri ya simu vilianguka. Ule uzuri wake nilijikuta mwanaume nikiviokota kwa kujituma kama vile me ndo nilisababisha aviangushe. Hawa watu wanaushawishi mazee 😄😄😄
Alitoa tabasamu akaniambia "hasante kaka Mungu atakulipa" nikasema usijali sister, wakaondoka.
Mda wa mimi kuondoka ulipofika nilipotaka kuondoka ndipo niliiona laini ya simu, nilihisi itakuwa ni ya yule dada niliiokota kama ingetokea ataitafuta nitampatia, nikasepa nayo.
Siku ya pili. Ilikuwa tunaanza vipindi bahati nzuri yule dada kumbe tulikuwa tunapiga masomo sawa, baada ya kipindi kuisha alisimama kama kuna mtu alikuwa anamtafuta aliponiona akaja kwangu alini salimia
"kaka mambo, sijui kama wanikumbuka siku ya orientation" kitanga hiko😂👆
Niliitikia kwa kutikisa kichwa, kwakuwa sikuwa mzoefu wa kuongea na wasichana wazuri nilijikuta namuuliza yule rafiki yako mzima? Bwana wee haya mambo😂
Aliitikia huku akikwepesha macho akauliza uliiokota laini yangu siku ile?
Nilimwambia ndio Nikamkabizi.
Yes, nilibahatika kujua jina lake, anaitwa Nadia😊😊, ndio Nadia Zubeir .
Urafiki wetu ulianzia hapa na labda ndo ulikuwa mwanzo wa matatizo nikiwa chuo 😩😩😩 Image
Urafiki ukakolea akiingia darasani anahakikisha ananitumia sms kama nipo kwenye kipindi. Pindi likiisha ananipitia tunasepa. Tukawa tunasoma pamoja na mara nyingi tulikuwa tuko pamoja. Binafsi nilishawahi kuwa na mpenzi lakini alikuwa hanijali hivi. Hawa watanga wanatumaliza 😂🙌
Urafiki wetu ulivoendelea siku moja nilimuuliza kuhusu yule mwana wa siku ya kwanza akasema hawafahamiani ni vile tu ucheshi wa yule mdada ndo maana walivokuwa wanapita nilidhani wanajuana.
Mwanaume nikaanza kumpenda yule mdada aise😍😍
Kiuhalisia mwanaume akipata mwanamke anaemjali huwa anapenda.
Nilianza kumpenda Nadia.
Alitokea familia bora kiuchumi kuliko yangu lakini nilivokuwa najitolea utadhani mimi ni mtoto wa Aliko Dangote.
Haya mapezi 😩😩😩
Kila weekend nilikuwa namtafutia zawadi nzuri
Nayeye kila alipokuwa anaenda kwao alikuwa akija na zawadi mingi. Wahuni wakaanza skendo kwamba manzi natoka nae kumbe hata huggs sijawahi pewa 😭😭😭
Maneno ya wahuni vile yanachoma boychild nikawa navumilia. Manzi akawa hashtuki hadi nikawa najiuliza au ananitaka nini.
Muhuni nikawa nasoma hadi natoboa night ilimradi kwenye pepa nisimuangushe manzi. Nikawa nampa company zote kwenye mtihani hadi akawa ananipita me mwenyewe.
Maneno ya wahuni yalipozidi nikaamua kumtongoza nijaribu bahati.
Akanichomoa bila kunipa sababu.
Aisee haya mambo 😥😥
Baada ya kumlazimisha sana akasema. Kwa tulipofikia hawezi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mimi. Tuwe marafiki tu. Kumbe ule mda wote tupo karibu me nazubaa wahuni walikuwa wanarusha nyavu. Tayari anamtu na wanamalengo yao tayari.
Wazee haya mambo😪😪
Basi bhna, kuona vile ikabidi nipunguze mazoea kwani kukaa nae karibu ingepelekea maumivu. Usiku ananipigia ananiuliza mbona kimya.
Nikawa namuambia tu niko busy kumbe moyoni najijua.
Akawa kila weekend ananilazimisha tutoke wote muhuni nakubali kishingo upande.
Tunaenda huko tunakula mavyakula tunarudi.
Nakumbuka siku moja ilinyesha mvua.
Ilikuwa tunasubiri daladala turudi chuo. Ilipita gari kwa kasi ikatumwagia maji machafu. Nikajifanya kupaniki nisionekane lofa kwa manzi.
Hii siku nilidundwa mbele za watu 😂😂😭😭 nacheka na inauma.
Aisee. Cha ajabu kipindi ambacho mimi napunguza mazoe manzi akawa ndo anachochea moto. Unajua nilitumia trick gani nimnase, sisi ndo wataalamu.
Nikamuundia mtego wa kizembe san.
Kunguru mjanja hunasa kwenye tundu bovu mazee😂😂
Next time nitaweka hapa ilikuwaje hadi kuachana na jamaa na kukubali kuwa na mimi. See you soon legends 😊👊
@Msumari9 Image
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Master

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!