My Authors
Read all threads
URI THE SURGICAL STRIKE:
Watu wengi wapenda filamu na hasa wale wanaopenda filamu za nguvu zenye actions za kumwaga, hawatapenda hata kidogo kuangalia filamu za Kihindi, lkn leo nataka niwaletee filamu moja ya kihindi ambayo Actions zake zinaacha nyuma filamu nyingi za kizungu, Image
na kutokana na ukali wake na actions zake kuwa kali na za kufurahisha HAKUNA MUDA WA KUIMBA WALA HAKUNA NYIMBO kwenye filamu hii, Kichapo kinaanza kuanzia filamu ilipoanza hadi inaisha (hivi si unajua kuwa ukiangalia filamu kali na yenye hisia kali
utaenda sana haja ndogo??) hii filamu itakupeleka chooni mara nyingi sana. Kama hujaona filamu hii sisi hapa #Cipherdotseriesandmovies tunakushauri (strongly recommend) Uione Hakika utatuambia Asante.
Uri ni filamu ya kihindi ya mwaka 2019 iliyoachiwa tarehe 11 januari, ikiwa ni Image
filamu ya Kivita iliyojaa actions kali za kijeshi (military Action film) pasipo mfano, kama umeangalia 13 Hours Secret soldiers of Baghanzi utanielewa nisemacho . Iliandikwa na Debutante Aditya Dhar na ikazailishwa na Ronnie Screwvala na wahusika wakuu wakawa
Vicky Kaushal, Image
Paresh Rawal, Yami Gautan. Mohit Raina and Kirti Kulhari .

Filamu hii inaegemea na kuongelea tukio la kweli lilowahi kutokea nchini India la kulipiza kisasi baada ya kifo cha Meja Karan wa Jeshi la india ambaye anakuwa muhusika mkuu kwenye tukio zima la filamu hii
Cfilamu hii iliyogharimu kiasi cha Dola za kimarekani zipatazo milioni 54) na ikaweza kupata mrejesho chanya kutoka kwa wakosoaji na wapanga viwango vya filamu na kuweza kujipati kiwango cha 8.3/10 katika viwango vya mtandao wa IMDb
Picha ilikuwa norminated kwenye Awards 15
na ilishinda Awards 8 ilizochaguliwa nazo ikiwemo ya National film Awards, ambayo ilijumuisha
Best director kwa Dhar and best actor kwa Kaushal

Picha hii imegawanyika ktk sehemu 5 zenye matukio na vipondo tofauti,

Sehemu ya kwanza ya filamu hii inayojulikana kama Wadada saba
(The Seven Sisters) inaanza na shambulio la kushutukiza lilofanywa na mgambo zidi ya msafara wa jeshi la India lililotokea mwaka 2015 mwezi june, katika msitu wa Chandel, Manipur, pia ktka sehemu hii tunaona pia kisasi cha shambulio hili la kushutukiza linalipizwa pale kikosi ImageImage
maalum kinachoongozwa na Vihaan kinapojipenyeza na kushambulia wanamgambo waliohusika na shambulizi la msafara wa wanajeshi wa india na kiongozi wao mkuu aliyehusika na shambulio hilo aliuawa siku hiyo.

Baada ya shambulio hilo kufanikiwa waziri mkuu wa india anampongeza Vihaan
na kikosi chake kwa kazi nzuri. Jambo la kusikitisha linatokea kwa Vicky pale mama yake anapokuwa anahitaji sana mtu wa kumlea kwa maana alikuwa na kansa ktk hatua za mwisho na hivyo kumfanya Vicky(vihaan) kuomba kustaafu ili akae karibu na mama yake.
Sehemu ya pili ya filamu hii Image
inajulikana kama Amani inayosuasua (An Unsettling Peace) inaaanza pale baada ya Vicky kukataliwa kustafu na kupewa kazi za ofisini. Na Vicky anaonekana akiwa na familia yake. Mambo mengi kwenye sehemu hii yanaongelea yale yanayotokea katk mauguzi ya mama yake Image
Vihaan na maisha ya ofisini na kisa cha mama yake kupotea...

India Ivuje damu kwa majeraha 1000 (Bleed India With Thousands Cuts) ni sehemu ya tatu ya filamu hii. Siku ya tarehe 18 septemba 2016 wanamgambo wanne wakiwa na silaha nzito walishambulia makao makuu ya
brigade ya Uri, na Jammu majira ya saa 9 usiku na kuua wanajeshi wa india wapatao 19 wakiwa bado wamelala ni kwenye tukio ili ambapo meja karan alifikwa na mauti baada ya kuonyesha ushuja wa hali ya juu ambapo alilipukiliwa na bomu lilotegeshwa na moja ya wavamizi hao. ImageImage
Kifo chake kiliumiza watu wengi familia yake pamoja na Marafiki. Kwa shambulio hili waziri mkuu alichukizwa na kuumizwa sana, Vihaan naye aliumizwa mno, waziri mkuu akaamua hatua kali za kijeshi kuchukuliwa kwa wale waliousika ama Image
kusaidia kutekelezeka kwa shambulio ilo.
wanamgambo hao ambao walikuwa wanajificha chini ya mwavuli wa Pakistan ndani ya kashmir iliyokuwa inashikiliwa na Pakistan. Mshauri wa usalama wa taifa wa India bwana Govind Bharadwaj akashauri kuundwa kwa kikosi cha kisasi alichokiita
SURGICAL STRIKE TEAM ambapo waziri mkuu aliidhinisha wazo hilo na kuundwa kwake na kuwapa siku 10 za maandalizi. Hapa tunamuona Vihaan akirudi kwa mkuu wake wa jeshi nakuomba kupewa nafasi ya kuongoza kikosi maalumu cha surgical strike ili kulipiza kisasi cha rafiki yake Karan Image
ambae pia alikuwa ni shemeji yake, Vihaan (Vicky) anapewa jukumu la kukiongoza kikosi hiki na anaacha kazi za kiofisi na kuhamia kambi ya jeshi iliyokuwa karibu na mpaka wa kashmir iliyoitwa Udhampur. Hapa Vicky anamuomba mkuu wa majeshi amruhusu mdada aitwaye Arjun Singh Rajawat Image
(Shishir Sharma) awe naye kwenye operesheni hiyo (huyu mdada alikuwa ruban mkali sana wa helicopta aliyejikuta akiwa mtu wa ofisini kwa kosa lisilo lake na ambalo asingeweza kulizuia)
Ruhusa ikatolewa mdada naye akawa ndani ya nyumba, kikosi cha kisasi kikaundwa kwa kuchagua Image
wanajeshi ambao ni makamando wapatao 80, wakali waliobobea kwenye mapigano ya kustukiza, wanajeshi wengi walichululiwa kutoka brigedi ile iliyovamiwa na kushambuliwa. Kikosi hiki kilianza mazoezi ya pamoja baada ya kuambiwa hawataweza kutumia simu toka siku hiyo hadi siku Image
watakayokamilisha kazi na pia hawakuambiwa lolote kuhusu dhumuni la zoezi hilo wala kazi hiyo waifanyiayo zoezi. Hii ilitakiwa iwe siri kubwa na kila kitu kilifanyika kwa usiri mkubwa ili upande wa pili usifahamu wala kugundua lolote wala kuhisi jambo lolote. Hapa ndipo filamu ImageImage
hii inaanza na ambapo mimi naishia hapa nisije kukukuharibia utamu wa kinachoenda kutokea mbele, ila cha muhimu cha kuzingatia nikuwa tarehe 28 Septemba 2016 ndo ilikuwa siku ya kazi HAKIKA hapa kiti hakitakuwa rafiki kwako maana hakitakalika na msalahani kwako atakuwa rafiki Image
wa karibu maana misisimuko utakayopata itakufanya upate haja ndogo pasipo kutarajia

Filamu hii ilikuwa nominated(kuchaguliwa) kwenye awards zipatazo 15 na iliweza kushinda awards 8 na kuingiza kiasi cha dola milion 15 kwa siku 8 za kwanza, na Dola milioni 31 zilipofika siku 15
na dola 45 ilipofika siku 28

Patakujua pia
Katika shambulizi la mgambo pale Uri mabomu 17 yalilipuliwa kwa dk 3, na wanajeshi 19 walikufa na 80 hadi 100 walijeruhiwa vibaya sana.
Ili kupata uhalisia wa mapambano ya kijeshi
Vicky na kikosi chake walipata mafunzo ya
ya kumiliki silaha na mafunzo mafupi ya kijeshi
Katika kambi ya mumbai naval base.
Vihaan(Vicky) alikuwa akifanya mazoezi kila siku kwa muda usiopungua masaa matano na masaa matatu alikuwa akipata mafunzo ya kijeshi ili kuweza kupata stamina ya kucheza uhusika wake. Image
Uzi huu umeletwa na Cipherdot Series and Movies waliopo DODOMA
filamu hii pia inapatika hapa kwetu ikiwa kwenye 1080p
Tupigie kwa namba zifuatazo
0767000650/ 0658000350
Tembelea pia page yetu ya instagram
instagram.com/Cipherdot_seri…
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Cipherdot Series And Movies

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!