My Authors
Read all threads
Thread:
TRUE STORY(Sitotaja miaka wala Majina);
Nikiwa chuo 1yr, nilikuwa na msichana ambaye alikuwa amemaliza form 4 akisubiria majibu, wa Dar. Mapenzi yalikuwa moto, nilikuwa nampunguzia boom langu kidogo aweze kujikimu mtaani maana familia yake uchumi sio mzuri sana.
👇🏾
Mwaka uliofuata matokeo yalitoka akapata Div 2, akaja kupangiwa Lugoba F5. Mapenzi yaliendelea kwa kuandikiana barua, na rafiki zangu wa karibu chuo walikuwa wanamjua vema na walikuwa wananipa Some ideas za kuandika kupamba barua. Rafiki yangu mmoja alikuwa ananichorea katuni.
👇🏾
Siku moja alipiga picha akiwa shule na kunitumia just nione uniform zao and how she looks akiwa kavaa uniform. Nilifurahi sana, nikamtumia picha yangu pia aone. Aliporudi likizo ya kumaliza F5 nilikuwa natumia boom kumpigia simu na kuongea nae. Ilikuwa hatupumziki kabsia.
👇🏾
Hiyo hali ilitufanya tuwe close zaidi na mapenzi yakawa maradufu zaidi, kipindi cha usiku tuliongea kwa masaa na weekends ndo balaa. Likizo ikaisha akarudi shule, tukaendelea kuwasiliana kwa barua Kama kawaida hadi alipomaliza form 6. Hadi kipindi hiki hatukuwahi kukutana.
👇🏾
Mwezi wa 6 huo mwaka matokeo yalitoka na alipata Div 2 tena. Wakati huo napiga msuli wa UE yangu ya mwisho. Nilipomaliza UE nikasepa zangu home, nikapanga niende Dar kuonana nae. Nikafika dar fresh na tukaonana kwa Mara ya kwanza, ilikuwa furaha kwetu sote.
👇🏾
Nilikaa dar siku 2 nikarudi Moro, baada ya kuonana ndo mtoto akawa anataka anipe mchezo na mie nilikuwa nautamani vibaya mno Ila ndo hivo nafasi finyu. Akaomba vyuo na mkopo, alifanikiwa kupata SUA ila mkopo alikosa kabisa. Mwezi wa 9 alienda kureport chuoni na kupata hostel.
👇🏾
Upande wangu nilipata kazi tayari na nikaanza kupokea mshahara, nilikuwa namsaidia pale anapokwama. Kiukweli sikuwahi kumnyima chochote kwa hali ya familia yake. Akiomba laki hata kama Sina nampa hata 40 ili apunguze makali ya chuo. Mambo yalikuwa safi hadi pale alipozoea chuo
👇🏾
Kipindi nimefanya nae mapenzi (alipomaliza F6) alikuwa bikra na ilikuwa kwangu Kama Zawadi maana ni nadra sana kuwakuta bikra wadada wa umri ule. Nilikuwa na Safari za kuja Moro nyingi tulikuwa tunaonana sana na kufanya yetu fresh. Marafiki zake chuo walikuwa wananijua fresh.
👇🏾
Zile Safari za kuja Moro mara kwa mara zikaisha. Hata semester moja haikuisha akaanza kuzingua, mimi nilikuwa nafanya kazi mkoa mwingine Kwahyo mara nyingi ni simu. Nasema alipozoea chuo kwasababu hakuwahi kuwa vile huko mwanzo ila mwanzo tu wa chuo akachange kabisa.
👇🏾
Akawa anaongea na simu usiku hadi saa 6, nilikuwa simpati kabisa. Nalala kesho yake namuuliza anasema sio yeye ni rafiki zake wanatumia simu yake. Tabia ikaendelea nikamwambia wakataze marafiki zako kutumia simu yako, akakubali. Siku 2 zikawa shwari ila tabia ikajirudia tena.
👇🏾
Sikulalamika tena, nikawa nataka kujua nini mwisho wake. Nikawa nampigia simu nakuta inatumika nalala zangu, kesho namsalimia asubuhi maisha yanaenda. Mambo yalibadilika haraka sana, mwaka huohuo aliojiunga chuo. Mwezi wa 12 kuna jamaa alinitafuta kwenye simu na kunichana live
👇🏾
Jina la mshikaji siwezi kulisahau kamwe, aliniambia “yule mwanamke ni wangu na hakutaki tena. Acha kumsumbua mwanamke wangu kumpigia simu usiku nikiwa naongea nae”. Sikuamini, nikampigia simu mdada akasema ni kweli, mimi simuwezi na namtia kwa kumuonea huruma kisa mdogo...
👇🏾
Wakati jamaa anamtindua hasa kiasi kwamba anashindwa kujizuia kuendelea nae. Nilijitahidi kumwambia jamaa na mdada kuwa wanachofanya sio sawa. Walinitukana wote kwa Pamoja na walinidhalilisha sana kiasi kwamba nilisema nitalipiza kisasi, ila baadae nikawa calm na kutulia.
👇🏾
Nikaendelea na maisha yangu, after 1yr nikiwa nishasahau Kila kitu na nishamove on. Dada wa yule msichana alinitafuta akisema amenikumbuk kaona anisalimie tu, nikaona sio shida fresh. After a week, mdada ananipigia simu ananisalimia pia. Nikamjibu vizuri nikasepa zangu.
👇🏾
Aliandika msg ndefu sana kujielezea, kwamba yule jamaa ni mwanafunzi mwenzake, na alikuwa nae kwasababu ya upweke kwakuwa mimi nilikuwa mbali. Na alimpa mimba mwaka uleule tulioachana na akamwambia hawezi kulea mtoto. Ikamlazimu ahairishe chuo hadi atakapojifungua. Ananipenda
👇🏾
Nikawaza haraka kwamba Huyu asingepatwa na majanga asingenitafuta. Nikamwambia tu pole sana kwa matatizo, ila mungu atakusaidia tu dada angu. Akaendelea kukazia kuwa ananipenda. Nilipekua kwenye siku yangu nikakuta namba ya yule jamaa yake. Nikamtumia msg zote za mdada.
👇🏾
Na nikamwambia, oya Hebu chukua takataka yako inanisumbua mimi. Baada ya dakika kadhaa, yule jamaa akanipigia. Akasema, mshikaji wangu usifanye hivo, sisi wote ni wanaume. Eti nisimuabishe kwakuwa Demu wake amenifuata tena, nikawambia hebu ongeza ufundi wa kumtindua Demu wako.
👇🏾
Wakapigiana simu huko, yule mdada akanipigia tena. Analalamika Kwanini nimemfanyia vile. Nikamwambia nimefanyaje, mimi sio msaliti eti niwe na wewe wakati namjua bwana ako. Nilichofanya ni kuwa mwema kwa bwana ako na kumwambia akushike na kukuhudumia vizuri. Alilia sana.
👇🏾
Nikaachana nae, akaanza kunitafuta Kila sehemu nikawa namchunia. Akarudigi tena chuo na akanipaga taarifa kuwa amerudi chuo, sikujibu. Ni miaka kadhaa imepita na huyo mwanamke Hadi Leo ananitafuta, alisema yuko tayari kuwa mchepuko wangu kwakuwa mimi ndo mwanaume anayemwamini.
👇🏾
Baada ya muda kidogo akawa anasema anataka kuolewa na Mimi. Anasema hajawahi kupata mwanaume kama mimi maisha yake yote. Nilimpenda mno Huyu mdada ila alichofanya kwangu ni kikubwa sana ambacho hakifutiki, na sitaki tena kufanya ujinga kwake. Nishamchunia sana ila haachi.
👇🏾
UKIPENDWA PENDEKA, maisha ni safari. Leo utamuona wa mbali ni kimeo kwa tamaa zako za mwili ila ukishavuruga pale mlipotengeneza kwa muda mrefu basi Huwezi tena kuparekebisha.
Watu wanawekeza kwenye mahusiano ila wenza wao wanaharibu.
NAWATAKIA KILA LA HERI KWENYE MAHUSIANO🙏🏾.
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Philipo Bethuel👨🏽‍💻

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!