My Authors
Read all threads
Thread:
USIDHARAU ANAYETAFUTA:
Rafiki yangu nimeonana nae kanisani leo akanipa stori, anasema amemuona professor flani ambaye alimdharau kipindi anatafuta kazi. Miaka 10 iliyopita jamaa alikuwa anatafuta kazi, akaongea na wazee wake wakaenda kuongea na huyo professor amsaidie.
👇🏾
Prof akasema kijana aende kwake na vyeti/CV aongee nae, jamaa akaenda mzee alipocheck tu vyeti vya mshikaji akamwambia kwa ufaulu huu kijana huwezi pata kazi kokote, akamwambia angalau ungekuwa na ufaulu **. Yale maneno yalimkatisha sana tamaa jamaa na kumvunja moyo kabisa.
Ili kutunza uhusiano mzuri na Prof hakuwaambia wazee kilichotokea kule. Akaendelea kutafuta kazi kwa mwaka mwingine mmoja bila mafanikio. Alikuja kupata kazi baada ya mwaka na nusu, jamaa alipanda vyeo kama upepo kutokana na utendaji wake wa kazi. Yuko stable kiuchumi sio mchezo.
Amekutana na yule Prof leo, alikuwa anapeana mikono na rafiki yake, Prof akamuona akamwambia “Heri ya Mwaka Mpya kijana”. Jamaa akaitikia fresh na kumwamkia. Prof akamuuliza Uko wapi siku hizi kijana? Jamaa akamwambia alipo na kazi anayofanya Hadi Prof akasema SAFI SANA KIJANA.
Aibu ilimtanda Prof kutokana na kauli alizotumia kwa jamaa akiwa hana chochote.
Nilimpa mkono rafiki yangu, nikamtakia Kila la heri kwenye maisha yake na yeye akanitakia heri, tukaagana.
Akapanda kwenye ndinga yake ya maana akasepa zake.
HAYO NDO MAISHA, USIKATE TAMAA💪🏾
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Philipo Bethuel👨🏽‍💻

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!